Vanessa Mdee awajia juu gazeti la babu kubwa. hiki ndo alichokisema. soma hapa

Thursday, June 13, 2013Mtangazaji wa Choice Fm, mwanamuziki, balozi wa vijana Tanzania, ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Gazeti la Babukubwa kuweka picha tofauti na walizokubaliana kwenye ukurasa wa mbele ambao ndio ukurasa wa mauzo wa gazeti (front page)
akizungumza na XXL jana vanessa amesema, picha iliyowekwa katika ukurasa wa mbele, sio picha iliyotakiwa kuwepo hapo, walipiga picha nyingi sana wakati wa session ya photo shoot, na kukubaliana picha zinazofaa kutoka lakini matokeo yake wametoa tofauti na makubaliano.
"tulikuwa tumeshachagua picha za front page na zile zitakazotokea ndani, za front page zilikuwa na version mbili na hakuna hata moja waliyoitoa, hata ukiangalia the headline, Ommy dimpoz ampata Vanessa, ukisoma tu unaelewa nini? ingawa story ni tofauti ndani lakini wangapi wanaliona gazeti na wananua kusoma kilichoandikwa ndani? aliuliza Vanessa.
it is so disrespectful, wanaharibu reputation, because my brand doesn't stand for that, wanaweza kukukosesha opportunities in the future.  
Soma zaidi

BALAA ....CHATU AKIWA AMEMMEZA MWANAMKE SIKU MBILI ZILIZOPITA HUKO DURBAN SOUTH AFRICA

Giant Snake Swallows woman in South Africa (See Photo)
Linda Laina Nyatoro, a South African reporter witnessed the incident and sent this picture. The giant snake swallowed a woman two days ago, near Durban North, South Africa.
Snake-300x300
Soma zaidi

Diamond Apata dili lingine


Wanasema hela huenda kwa wenye hela na mwenye nacho huongezewa zaidi. Sina uhakika, lakini
kwa mujibu wa picha nilizoziona kwenye akaunti ya Instagram ya Diamond 
Platnumz, inaonekana kama the lad is about get some serious money from 
wazee wa machapati ‘Azam’.
Katika akaunti hiyo, Diamond ameweka 
picha kadhaa ambazo zote zinamuonesha akiwa amebeba magunia ya unga wa 
ngano wa Azam na katika picha moja ameandika, “Guess what???.
Tutegemee surprise siku si nyingi!
Soma zaidi

Mwanaume kwa mwanaume wafumaniwa wakivunja amri ya 6 gesti.


WIKI chache tangu gazeti hili liliporipoti habari iliyohusu mume wa mtu kunaswa gesti na mwanaume mwenzake, mapema wiki hii, ile Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ chini ya Global Publishers imenasa timbwili lingine la aina hiyo gesti.
Tukio hilo lilishuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi wa Global ambapo mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanamke: Haloo haloo! Nazungumza na mwandishi wa Global?
 Mwandishi: Ndiyo, dada tukusaidie nini?
Mwanamke: Naomba msaada wenu jamani, nataka kumfumania mume wangu ana tabia chafu sana!
Mwandishi: Tabia gani?
Mwanamke: Anafanya vitendo vya kishoga na leo amepanga kukutana na huyo mwanaume mwenzake gesti (akiitaja) iliyopo Kinondoni, nimeona meseji walizokuwa wakichati.
Mwandishi: Unaweza kuja ofisini kwetu ili tupange namna ya kuwafumania?
Mwanamke: Si hapo Bamaga?
Mwandishi: Naam.
Mwanamke: Kwa kuwa nipo mitaa hii ya Kijitonyama nakuja sasa hivi.
Baada ya nusu saa mama huyo alitinga Makao Makuu ya Global, Bamaga-Mwenge na kuweka kila kitu wazi ambapo kikosi kazi kilijiandaa kwa ajili ya kazi hiyo.
FUMANIZI
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
WANAUME WATINGA GESTI
Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.

MKE, POLISI, WAANDISHI WATINGA NDANI
Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.
Kufuatia timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimbua mbio mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.

credt: GPL
Soma zaidi

"Nikifa Asha Baraka asije kwenye msiba wangu".....Ally Choki

Tuesday, June 11, 2013MKURUGENZI wa Extra Bongo Ally Chocky ametoa kauli nzito kuhusu waajiri wake wa zamani, Asha Baraka na Baraka Msilwa.

Katika maongezi yake  Chocky alisema katika watu asiowapenda duniani ni Asha Baraka (Mkurugenzi wa ASET) na Baraka Msilwa (Mwenyekiti wa ASET). Asha Baraka na Baraka Msilwa ni mtu na kaka yake.Kiongozi huyo wa Extra Bongo akaenda mbali zaidi kwa kusema: “Nikifa leo hii Asha Baraka na Baraka Msilwa wasije kwenye mazishi yangu, na kama watanitangulia wao na mimi sitakwenda kwenye mazishi yao.

“Nina uhakika leo hii nikipata matatizo au nikifa Asha na Msilwa watafurahi, sasa kuna haja gani ya watu kama hao kuja kwenye mazishi yangu.

“ASET ni kama simba wako tayari kukutafuna hadi macho, nimetafakari kwa muda mrefu sana nimevumilia mengi sana lakini nimeshindwa na sasa natamka rasmi, Nikifa wasinizike.”

Chocky ameorodhesha sababu nyingi sana za kufikia hatua hiyo lakini miongoni mwa sababu zake ni hizi tatu:

Kwanza kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari, pili Aset kukataa kurudisha pesa za Miraji Shakashia na tatu ni ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia pesa nyingi.

Chocky ansema kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana.

“Mtu anapokupeleka mahakamani maana yake ni kwamba yupo tayari hata ufungwe, ukifungwa maana yake ni kila kitu kwenye maisha yako kinaharibika.

“Gari walinipa wenyewe na maandishi yapo kwamba nikimaliza mkataba wangu gari litakuwa la kwangu.

Lakini badala yake wakanigeuzia kibao na kwenda kunidai mahakamani kwamba nimeiba gari.

Kuhusu Shakashia, Chocky amesema mwanamuziki huyo alichukua shilingi milioni tano za Extra Bongo ili ajiunge nayo na akasaini mkataba wake.

“Lakini badala yake Shakashia akaingia mitini na pesa zetu, Aset wakasema watazirudisha wao na sasa wanakuja na hadithi mpya.

“Wanasema hawawezi kurudisha hizo pesa eti kwa vile wananidai, wanasahau kuwa mkataba wa Shakashia ni kati yeke na Extra Bongo na sio Ally Chocky.

“Hata kama kipo wanachonidai hiyo ni kati ya Chocky na Aset na haiingii akilini kuliingiza suala la Shakashia ndani yake.

“Huu ni utapeli na inatoa picha kuwa Aset walimtumia Shakashia kufanya utapeli huu, lakini wajue kuwa mwisho wa siku atakayeathirika ni Shakashia mwenyewe,” alisema Chocky.

Kuhusu kutothamini wasanii waliozalishia pesa nyingi kampuni, Chocky anasema wasanii walipota ASET na kuizalishia pesa hawana chochote walichopewa kulingana na thamani ya kile walichokizalisha. “Sio pesa tu bali hata heshima pia hakuna,” alifafanua Chocky.

Chocky akazama zaidi na kuwataja wakongwe kama Shem Karenga na Kasongo Mpinda ambao waliwahi kufanya kazi katika familia ya kina Asha Baraka kupitia bendi za MK Group na MK Beats.

“Wako wapi Kasongo Mpinda na Shem Karenga, Kasongo aliwatengenezea pesa nyingi kupitia MK Group “Ngoma za Magorofani” huku Shem Karenga  akiwatengenezea utajiri katika MK Beats “Tukunyema”.

“Lakini hebu tujiulize wako wapi hawa wazee na wana kipi cha kujivunia?” alihoji Chocky.
 
 Haikuishia hapo, tuliamua kumpigia Asha Baraka ambaye naye alikuwa na yake ya kujibu kuhusu  mapigo ya Chocky.

Asha Baraka amesema hayo ni mambo ya kike na kwamba kuzikana si tija.

Asha Baraka akasema: “Hata mimi sina mpango wa kwenda kwenye mazishi yake na yeye pia asije kwenye mazishi yangu.

“Hivi kuzikana ni nini? Wazazi wangu walifariki na Chocky hakuja kuzika, kilipungua nini? Halafu mi nikifa sitaona na yeye akifa sitaona kwahiyo hiyo siyo ishu, wamanyema wenzangu watatosha kunizika hata wasanii wote wasipokuja achilia mbali huyo Chocky.

“Nilimzikia wazazi wake na hakuliona hilo kwahiyo hata tusipozikana hakipungui kitu.

“Chokcy tunamdai gari na pesa shilingi milioni 13, kwenda mahakamani ni sehemu ya kudai haki na yeye kama anaona amedhulumiwa kuhusu pesa za Shakashia basi aende mahakamani.”

Asha Baraka alimtaka Chocky aelewe kuwa baadhi ya wasanii wa Twanga ni virusi na watammalizia pesa zake bure.

“Wako wasanii wamelelewa vizuri, wamefanyiwa mengi na Twanga na wanaelewa utu kwahiyo akijipendekeza kwao atapoteza pesa zake bure.

“Hao ni virusi wetu, wanatuletea taarifa zote za kila mtu anapotaka kuwachukua.


Asha Baraka amesema kama ni roho mbaya Chocky ndio anaoongoza kwa roho mbaya.

“Alikaa yeye na kamati yake yenye wakiwemo mpaka wafanyakazi wa umma na kuzoa wanamuziki wa Twanga”

Anawataja wasanii wa Twanga waliowahi kuchukuliwa na Extra Bongo ni pamoja na Ferguson, Rogart Hegga, Hosea, Otilya, Nyamwela, Danger Boy, Aisha Madinda, Maria Soloma, Subrina pamoja na Kanuti ambaye baadae alirudisha pesa zao na kubakia Twanga.

Asha Baraka anawataja wasanii wengine wenye damu ya Aset ambao wako Extra Bongo ni Ephraim Joshua, Martin Kibosho, Athanas, Banza Stone na yeye mwenyewe Chocky.

“Kwa mfumo huo utaona wazi kuwa Extra Bongo inapumua kwa nguvu ya Aset lakini sisi hatujasema kitu, kama ni kutoa kauli ya kutozikana basi sisi ndio tulipaswa kuwa wa kwanza,” alifafanua Asha.

“Tunajua pia kuwa Chocky alihusika kushawishi usajili wa Chaz Baba Mashujaa Band akiamini kuwa kwa kuondoka Chaz Twanga itakufa,” aliongeza

Asha Baraka amemtaka Chocky aonyeshe mfano wa namna ya kulea wasanii kwa kuwapa maisha mazuri wanamuziki waandamizi kama Banza na Rogart.

“Asiangalie mambo ya Aset, ajitazame yeye anaishi vipi na Banza anaishi vipi, badala ya kutoa milioni tano kumnunua Shakashia, angemnunulia japo Corola Banza au Rogart.

“Chocky aitishe mkutano wa waandishi wa habari halafu mimi na yeye twende na mikataba ya wasanii inayoonyesha mishahara na marupurupu tuone nani analea vizuri wasanii.

“Mimi nilifanya kazi Bima na sijajengewa nyumba wala kununuliwa gari, silalamiki kwa kuwa haikuwa sehemu ya makubaliano yetu.

“Kama Chocky anadhani muziki unalipa kiasi cha kumnunulia kila mtu gari na nyumba basi atuonyeshe mfano kupitia Extra Bongo.

“Kila baya linalomfika basi mchawi ni Aset, mbona mimi naumwa mguu na sijawahi kusema ni Chocky?

“Chocky akapime afya yake apate ukweli, tunajua rekodi ya sehemu alizopita, sasa asije akadondoka akasema ni Aset …akapime kwanza” alimaliza Asha Baraka.
Soma zaidi

Picha 8 za mazishi ya msanii wa bongo movie ( Kashi )

 
 
 
 
 
 
 
Pichani juu ni mazishi ya msanii ya mwigizaji  Jaji Khamis 'Kashi' aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar yaliyofanyika leo mchana majira ya saa nane kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Marehemu Kashi alikumbwa na umauti baada ya kuugua ghafla malaria na kifua. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Kashi mahali pema peponi. AMEN!
Soma zaidi

Sitaki kubishana na msanii yoyote wananjaa "Ney wa mitego" soma zaidi alichokisema Nay wa mitego
Rapper
Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya
wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya
wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo
huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio
anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha, mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo, kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa, kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho ntawaajiri wasanii wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za kufanya." amesea Ney.
Soma zaidi

Jaguar aendelea kuthibitisha ni jinsi gani ana mshiko wa kutosha, lakini hasau kondom anaposafiri

Ulikuwa bado una wasiwasi na utajiri wa msanii wa Kenya Jaguar? Well, sio mimi ni yeye ndio katoa tip ya kile alichokuwa amebebea jana jioni kabla ya kupanda ndege kurudi nchini Kenya akitokea UK.
Jaguar
Katika picha aliyoiweka kulikuwa na Passport yake ili wasije kusema alitumia picha ya mtu mwingine, then cheni moja ya gold ya hatari, saa mbili za gharama, Samsung Galaxy note, Calvin Klein Cologne na noti za UK pound za kutosha.
Lakini Jaguar amedhihirisha hana kigeugeu katika swala zima la kujilinda, alikuwa na pakti moja ya condom aina ya durex, nadhani hii ndio iliyobaki, LOL!.
Hit maker wa ‘Kigeugeu’ Jaguar alikuwa akirejea Kenya baada ya kuvuka boda kama alivyoimba katika wimbo wake ‘Navuka boarder’ akitokea London Uingereza ambako alitumbuiza katika show moja na TID wa Tanzania.
Soma zaidi

Kua wa kwanza kucheki picha za show aliyopiga Jaguar na TID huko Uingereza.

Soma zaidi
 
Copyright © 2013. NJE NDANI - All Rights Reserved